June 28, 2018



Sasa ni uhakika kwamba Simba imeamua hasa kuachana na Juuko Murshid.

Murshid aliamua kukaa kimya bila ya mawasiliano yoyote na uongozi wa Simba ambao pia uliendelea kumsaka bila ya mafanikio.

Taarifa za awali zilieleza kwamba Simba waliona wangeweza kuzungumza na Juuko na kuona kama ingewezekana kuongez mkataba.

“Hii ya safari hii imetuchosha sasa, inakuwa kama yeye ni mkubwa kuliko klabu jambo ambalo safari hii, halina nafasi.

“Tumemtafuta sana, amekuwa kimya. Haelezwi kitu na tunaona imekuwa too much. Hakuna atakayembembeleza, niwaambie ukweli sasa ni moja kwa moja, hakuna kujiuliza tena. Juuko ndiyo kaondoka hivyo,” kilieleza chanzo.

Mara kadhaa, uongozi wa Simba ulikuwa ukitaka kumuacha Juuko lakini ukawa unasita kwa hofu kuwa ni kipenzi cha mashabiki.

1 COMMENTS:

  1. Hana maadili mazuri. Mchezaji mzuri lakini nidhamu yake bado. Aende tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic