June 28, 2018





Pamoja na kuwa na taarifa Yanga imeanza usajili lakini suala la madeni ya wachezaji, inaonekana kuuchanganya uongozi wa Yanga.

Uongozi wa Yanga umeshindwa kufanya usajili muendelezo kutokana na madeni ya aina mbili ya wachezaji.
“Si kazi rahisi ndugu yangu, ukiwa nje ya Yanga unaweza kuona ni mambo rahisi lakini tunapambana sana na tunaumia pia.

“Kabla ya usajili tunatakiwa kupanda milima miwili. Kwanza tulipe madeni ya usajili ya baadhi ya wachezaji. Halafu ufuatie mlima wa pili ambao ni madeni ya mishahara,” kilieleza chanzo cha uhakika.

“Baada ya hapo unaweza kuzungumzia suala la kusajili mchezaji mpya. Ingawa kwa hali inavyokwenda, tunaweza kuanza tu usajili.”

Tayari Yanga walichagua kamati maalum ambayo ilipitishwa na wanachama. Taarifa zinaendeleza, kamati hiyo inataka kufanya usajili badala ya suala la madeni.

Imeelezwa, kamati hiyo chini ya Abbas Tarimba imetaka kusimamia usajili mpya na uongozi ufanye kazi ya kulipa madeni yake.


2 COMMENTS:

  1. Viongozi Yanga mnajitahidi sana isipokuwa mngechezesha hata timu B kwenye KAGAME pesa ingeingia kuliko kukaa bila mechi wachezaji huku wanadai.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Akili halisi ya kitanzania! Hivi hicho kiingilio cha Kagame kinaweza kukidhi haja ipi katika ulipaji mishahara? au hao wachezaji wa timu B maandalizi yao yatakuwa upepo na wao ni robot?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic