June 29, 2018


Baada ya kuwatambulisha Meddie Kagere, Pascal Wawa na Deogratius Munish jana mbele ya Waandishi wa Habari, uongozi wa klabu ya Simba umesema utaendelea na usajili wa wachezaji wengine.

Simba wamesema wataendelea kusajili kulingana na mashindano mengi ambayo wanakabiliwa nayo huku wakichagizwa na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya klabu hiyo, Haji Manara, amesema watazidi kufanya hivyo kwani hawana lengo la kumfurahisha mtu bali ni mipango ya dhati kuhakikisha Simba inakuwa na kikosi kipana pia kufanya vizuri.

Manara amesema Simba itakuwa na mashindano mengi ambayo ni Ligi Kuu Bara, Kombe la Mapinduzi, Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam Sports Federation CUP, SportPesa Super CUP na KAGAME hivyo ni lazima wawe na kikosi kipana.

Aidha, Manala amesema Simba inapaswa kutekeleza agizo la Rais Magufuli ambaye aliomba klabu hiyo iwe ya kwanza kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika au walau iweze kufika fainali ya mashindano hayo.

1 COMMENTS:

  1. Safi sana ila ili Simba ikate mzizi wa fitina lazima kuwepo na uti wa mgongo imara wa timu yaani beki imara,kiungo imara ws level ya kimataifa,fowadi imara,ambapo wawa naweza kusema ni mtu sahihi. Lakini lazima wapatikane kiungo wa kazi kweli kweli na kama atakosekana basi itabidi wamuandae shomari kapombe kuwa kiungo wa kudumu na wampe majukumu yote kikamilifu katika dimba la kati. Simba baada ya kumsajili Meddie Kagere kule mbele kumekaa vizuri sasa. Matumaini yetu viongozi wa simba hawatapuuza ushauri mbali mbali wa wadau wa soka nchini kwani Simba imebeba matumaini ya watanzania waliowengi hata muheshimiwa raisi kunako kuelekea kwenye mashindano hasa ya Africa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic