June 29, 2018


Kocha Mkuu wa Singida United, Hemed Morocco, ametoa kauli ya kishujaa kwa kusema kuwa, licha ya Simba kuendelea kufanya usajili mkubwa, lakini hawaihofii wakikutana kwenye michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza leo Ijumaa jijini Dar.

Simba ambayo inaendelea na usajili, hivi karibuni ilitangaza kumsajili Meddie Kagere kutoka Gor Mahia ya Kenya am­bapo kwenye Kagame, Simba na Singida zimepangwa kundi moja la C.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Morocco alisema kwa mwaka huu wanataka kushinda kila kitu, hivyo wanaanza na Kagame.

“Tunataka kushinda kila kitu, hayo ndiyo malengo yetu na ndiyo maana tuko watulivu katika usajili.

“Tunataka kutumia mashindano ya Kagame kwa mambo matatu, kwanza kushinda kila mechi na kut­waa ubingwa, pili ni nafasi ya wache­zaji wetu kupata uzoefu wa mechi kubwa, na tatu ni kupata muungan­iko mzuri wa wachezaji wetu kabla ya kuanza kwa ligi.

“Tupo kundi moja na Simba, wala hatuihofii, tumejipanga kupambana nayo na timu nyingine zote tutaka­zokutana nazo,” alisema Morocco.



2 COMMENTS:

  1. Morocco unakosea. Ya Simba wewe hayakuhusu. Muhimu andaa vijana wako wacheze kutafuta ushindi. Kwani Simba atachezesha wachezaji 20 au 11 wakati wa kucheza? Huo ndio uwoga wenyewe unapoanza kuzungumzia timu nyingine kusajili hayakuhusu.

    ReplyDelete
  2. Kocha Morocco mbona nakuamini umefanya mambo makubwa, kwani Simba wamefanya usajili kwa ajili ya kupambamana na Singida United ama wenyewe wanaimarisha kikosi chao?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic