June 24, 2018



Kocha Mkongomani wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amewakingia kifua wachezaji wake kuhusiana na kujitoa kwenye mashindano ya KAGAME inayotarajiwa kuanza Juni 29 wiki kesho.

Zahera ambaye alikuwa kwao Congo kwa likizo maalum, amewasili nchini tayari kuwasubiri vijana wake wanaotarajiwa kuanza kuwasili kesho baada ya kumaliza mapumziko.

Kocha huyo amefunguka na kusema Yanga iliamua kuomba kujiondoa KAGAME kutokana na wachezaji wenyewe kuomba mapumziko ili waweze kutuliza akili zao kuja kujiandaa na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Zahera ameeleza kuwa wachezaji walikubaliana na uongozi wao kisha wakatuma maombi kupitia barua kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyoomba kujiondoa mashindanoni.

Yanga itakuwa ina kibarua nchini Kenya dhidi ya Gor Mahia FC Julai 18 na maandalizi ya mechi hiyo yataanza mapema wiki ijayo mara baada ya kuwasili kambini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic