BARCELONA YAZIFUNIKA VIBAYA MAN UNITED NA MADRID
Barcelona imetajwa kuwa klabu ya soka inayoongoza kwa kuingiza fedha nyingi kutokana na malipo ya udhamini, ikiwa inaingiza pauni 187m kwa mwaka.
Barcelona inaingiza pauni 35m zaidi ya Manchester United na pauni 37m zaidi ya Real Madrid ambazo ndizo zinazofuatia katika orodha hiyo.
Mapato yao mengi yakitoka kwa Nike ambao wana mkataba nao wa pauni 88m kwa mwaka unaotarajiwa kudumu hadi mwaka 2023.
Taarifa iliyotolewa na Jarida la Forbes imeelezwa Chelsea inashika nafasi ya nne ikiingiza pauni 102m, ikifuatiwa na Bayern Munich (pauni 91m), Paris Saint-Germain (pauni 76m).
Nyingine ni Arsenal (pauni 71m), Liverpool (pauni 70m), Tottenham (pauni 61m) na Manchester City (pauni 59m).
0 COMMENTS:
Post a Comment