June 30, 2018


Na George Mganga

Ukiwa ni mwezi mmoja umesalia kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba kufanyika, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, bado hajafanikiwa kukutana na wanachama waliokuwa wanapinga mabadiliko ya katiba mpya ya Simba.

Ikumbukwe katika mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika mara ya mwisho kwenye ukumbi wa JK Nyerere, Posta, Dar es Salaam, Mwakyembe alisema atakutana na wanachama hao ili waweze kuzungumza na kufikia mwafaka juu ya suala la katiba ambayo ipo kwenye mchakato wa kusajiliwa na serikali hivi sasa.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia kipindi cha Spoti Leo, Mkurungenzi wa Wizara yenye dhamana ya Michezo, Yusuph Omary, amesema kuwa wanachama hao bado hawajakutana na Mwakyembe kutokana na kukabiliwa na majuku ya kikazi.

Omary amesema Mwakyembe anakabiliwa na kazi nyingi za kiserikali hivyo ameshindwa kukutana na wanachama hao ambao wamekuwa wakienda tofauti na matakwa ya wanachama wengi ambao wameafiki katika ya Simba iweze kubadilishwa ili kuruhusu mfumo mpya wa uendeshaji.

Mkurungenzi huyo amesema wanachama hao walitinga ofisini na kuepeleka nakala iliyokuwa inahoji kuhusiana na uchaguzi huku wakihoji kuhusiana na suala la katiba ambapo wamekuwa wakiiunga ile ya mwaka 2014 tofauti na ya 2016.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic