June 27, 2018





Mshambuliaji aliyewahi kuichezea Manchester City ya England, Wilfred Bony raia wa Ivory Coast ametua nchini hivi karibuni kwa ajili ya mambo mbalimbali yakiwemo kutoa msaada kwa watoto wanaishi katika mazingira magumu, kuwekeza katika muziki pamoja na kujikita katika kuinua soka la vijana.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano katika Hoteli ya Protea iliyipo jijini Dar, Bony ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea Swansea City iliyoshuka daraja amesema kwamba uwepo wake hapa utasaidia katika sehemu hizo ambapo kwenye muziki anatarajia kwa kushirikiana na wadau wa hapa kwa kujenga kituo kitakachohusika na masuala hayo.


"Hii ni mara ya pili mimi kuwepo hapa, nilikuja miaka mitano na timu ya taifa ya Ivory Coast, lengo kubwa ni kuja kusaidia jamii na tumefanya hivyo japo sihitaji kujitangaza kwamba ninasaidia.


"Lakini pia tutagusa katika kuwekeza kwenye muziki kwa kujenga kituo ambacho kitajihusisha na masuala hayo. Mimi nawasikiliza sana Diamond, AliKiba, Linnah na wengine ambao siwajui majina.


"Na mwisho tutawekeza katika kuibua na kuwasaidia vijana wadogo wanaocheza soka waweze kufikia malengo yao ya kuwa nyota wakubwa kama ilivyo kwetu sisi," alisema Bony.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic