June 27, 2018


Imeelezwa uongozi wa Gor Mahia FC umeshangazwa na kitendo cha mshambuliaji wao tegemeo, Meddie Kagere kujiunga na klabu ya Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Wakati Kagere akiwa nchini Kenya ikiwa ni wiki kadhaa zimepita baada ya mashindano ya SportPesa Super Cup kumalizika, aliomba ruhusa kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya masuala yake binafsi.

Lakini kilichokuja kuwashangaza ni Kagere kuchukua ndege ya kuelekea jijini Dar es Salaam akiwa na wakala wake kwa ajili ya kuja kufanya mazungumzo na Simba kisha kusaini mkataba wa miaka miwili.

Kitendo hicho kimewaumiza Gor Mahia na kuona kama Kagere ni msaliti wakati walikuwa kwenye mazungumzo naye ya kuongeza mkataba mwingine baada ya ule aliokuwa anao ndani ya klabu hiyo kumalizika.

Aidha, imeelezwa viongozi wa Gor Mahia wameshangazwa na Kagere kushindwa kuwaeleza hali halisi kuwa alikuwa anataka kusafiri kuelekea Tanzania na badala yake alidanganya kuwa anaenda kwao Rwanda.

Tayari Kagere ni mali ya Simba na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi hicho katika michuano ya KAGAME inayotaraji kuanza Juni 29 2018.

7 COMMENTS:

  1. Gormahia wamejitakia kutokana na kauli zao za dharau kwamba club za Tanzania hazina uwezo wa kuwachukuwa wachezaji wao. Walivyofanya SIMBA ni safi kabisa kabisa. Na hata yule kiungo wao rasta kama kungekuwa na nafasi zaidi ya wachezaji wa kigeni basi Simba ingemchukua tu ili kuwatia adabu hawa wakenya kuwa na kauli za kiungwana badala ya kejeli na dharau kwa watanzania.

    ReplyDelete
  2. Vipi wanamwita msaliti ambapo mchezaji mkataba wake umeshamalizika na hakuna hela aliyopokea au kuahidi atabakia Gor. Huyo ni mchezaji huru na sio mtumwa wao anatazama maslaha yake au ndio mlifikiri Simba haina haki au uwezo wa kumnyakuwa kwa sheria za mpiraa. Msidharau uwezo wa Mo

    ReplyDelete
  3. Mechi na Yanga itakuwa na unafuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mechi ipi na Yanga? Wamejitoa Kagame. Mpaka Ligi kuu ndipo tukutane.

      Delete
  4. watajuta kuzaliwa kenya
    kagere kalibu kwa mnyama wa Tz

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic