Klabu ya Simba imefanikiwa Kumleta nchini beki wa zamani wa Azam FC Paschal Wawa kwaajili ya kumsainisha mkataba wa kuitumikia timu hiyo na tayari ameshaanza mazoezi kujiandaa na michuano ya kagame inayoanza kutimua vumbi june 28 mwaka huu.
Wawa ameanza mazoezi leo Juni 25 na kikosi cha Simba ambapo awali alishawahi kucheza Azam msimu wa 2015-2016 baada ya hapo alitua nchini Sudan katika klabu ya El Merekh ambayo ameitumikia kwa msimu mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazoezi hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Boko Veteran Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema kuwa wanaendelea na mazoezi huku wakiwapumzisha baadhi ya wachezaji wao wakubwa.
Ujio wa Wawa katika kikosi cha Simba ni katika hali ya kukisuka kikosi hicho ambacho baadae mwaka huu kitashiriki michuano ya klabu bingwa Afrika na Msimu mpya wa ligi kuu pia kombe la Kagame linaoanza juni 28 mwaka huu.
Kutoka Global TV
Jamaa amekaa kibabe kwa beki umbile lake safi saana.
ReplyDeleteHeee haji tena Yanga?
ReplyDeleteni vyema kuchanganya kikosi ila tutahadharishe tu kwamba ukijaza wachezaji wa kongwe kiumri unajitafuatia hatari kdg maana majeruhi yanaweza kusumbua sana kikosi
ReplyDelete