Chelsea wamekataa ofa kutoka Barcelona ya paunia milioni 50 kwa kiungo wao wa kati raia wa Brazil William. (Mail)
Manchester United pia nao wanatarajiwa kutoa ofa yao kwa William wakati menaja Jose Mourinho anajaribu kumsaini mchezaji wake wa zamani huko Chelsea. (Express)
Tottenham hawatamuuza mchezaji wao yeyote kwa kikosi cha kwanza hadi baada ya kurudi kutoka likizo kufuatai kombe la Dunia. (ESPN)
Kipa Simon Mignolet, 30, atafanya mazungumzo na Liverpool baada ya kampeni ya Ubelgiji ya Kombe la Dunia wakati anataka kujua kama atapata fursa katika kikosi cha kwanza msimu ujao. (Guardian)
Everton wanajiandaa kutoa ofa ya pauni miloni 25 kwa beki wa Celtic msikochi Kieran Tierney, 21. (Telegraph)
Everton wametoa ofa mpya kwa mlinzi mwenye miaka 29 raia wa Croatia Domagoj Vida na wanatarajiwa kumbadlisha na kiungo wa kati mholanzi Davy Klaassen 25, (AMK Spor via Sport Witness)
Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anataka kumsaini wing'a wa Chelsea Kenedy, 22, na mchezaji wa Red Bull Salzburg mwenye miaka 25 raia wa Kosovo Valon Berisha katika hatua ambayo itagharimu pauni miloni 35. (Telegraph)
Kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23, amehusishwa na kuahama kwenda Manchester United lakini anasema ana furaha ikiwa atabaki Lazio na atachukua muda kupumzika kisha aamue baada ya nchi yake kutupwa nje ya Kombe la Dunia. (Express)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment