June 30, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, Kocha wa Gor Mahia FC, Dylan Kerr, amemuulizia aliyekuwa straika wake Meddie Kagere.

Kocha huyo ameulizia kama Kagere kama atacheza mchezo wake wa kwanza leo dhidi ya Dakadaha ya Somalia ambapo Simba watakuwa wanafungua pazia la michuano hiyo kuanzia saa 8 mchana.

Kerr anaonekana kuumizwa na kitendo cha mchezaji huyo kunaswa na mabosi wake wa zamani kutokana na kuukubali uwezo wa Myarwanda huyo mwenye asili ya Uganda baada ya kufanikiwa kumnyakuwa na kumsanisha mkataba wa miaka miwili.

Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa Kagere hatokuwa sehemu ya kikosi cha Simba leo baada ya kurejea Kenya kukamilisha baadhi ya mambo na uwezekano wa kucheza utakuwe siku ya Jumatatu ambapo Simba itakipiga na APR ya Rwanda.

Tayari Gor Mahia imeshawasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano ya KAGAME ambayo yameanza rasmi jana kwa mechi tatu kuchezwa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic