DALALI ATOA ELIMU FUPI KUHUSIANA NA UTANI WA JADI KWA SIMBA NA YANGA
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Mzee Hassan Dalali, amefunguka na kueleza dhana nzima ya utani wa jadi baina ya timu za Kariakoo (Simba na Yanga).
Dalali amejaribu kugusia suala hilo wakati akizundua tawi jipya la Simba maeneo ya Kawe jijini Dar es Salaam leo.
Dalalo ameeleza kuwa Simba na Yanga ni marafiki na ni ndugu hivyo hakuna haja ya kuchukiana wala kutukanana na upinzani wa timu hizo mbili unakuwa ndani ya dakika 90 pekee.
Akizungumza kupitia Radio EFM, Mwenyekiti huyo wa zamani ameamua kufunguka hayo kutokana na baadhi ya mashabiki wasiolewa maana ya utani wa jadi ili kuweka mambo sawa.
"Sisi kwa pamoja si maadui bali ni watani, upinzani wetu unapatikana ndani ya Uwanja tunapopigania dakika 90 kupata matokeo, baada ya hapo tunakuwa marafiki ambao tunashirikiana kwenye mambo mengi" amesema Dalali.
Zac
ReplyDelete