June 24, 2018


Dakika 90 zimemalizika katika mchezo wa Kombe la Dunia kwa Senegal kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Japan.

Walikuwa ni Senegel walioanza kuziona nyavu za Japan kupitia kwa Sadio Mane mnamo dakika ya 11 ya kipindi cha kwanza na baadaye Japan wakasawazisha kupitia kwa Takash Inui kwenye dakika ya 34.

Mpaka dakika 45 za kwanza, Senegal na Japan walikuwa sawa kwa idadi hiyo ya mabao 2-2.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi baina ya timu zote mbili kushambuliana kwa zamu na katika dakika ya 71 tena Senegal wakaongeza bao la pili kupitia kwa Moussa Wague.

Ilichukua takribani dakika 8 kwa Japan kuweza kusawazisha kupitia kwa Kisuke Honda aliyemalizia krosi safi ambayo ilishindwa kudhibitiwa na mabeki wa Senegal.

Msimamo wa Kundi H unaonesha Japan wameshika nafasi ya kwanza na Senegal wakiwa wa pili kutokana na utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic