June 25, 2018


Na George Mganga

Wakati michuano ya Kombe la Dunia ikiendelea kushika kasi nchini Urusi, nikujuze machache ambayo yawezekana ulikuwa hauyafahamu.

Mshambuliaji Harry Kane anayichezea timu ya taifa ya England jana amefunga mabao matatu katika mchezo mmoja maarufu kama Hattrick na kuungana na wakongwe kama Gary Lineker pamoja na Geoff Hurst waliowahi kufanya hivyo pia.

Kane amekuwa mchezaji pekee aliyefunga mabao mengi mpaka sasa kwenye michuano hiyo, amefunga matano huku Cristiano Ronaldo kutoka Ureno na Romelu Lukaku wa Ubelgiji wakifunga manne kila mmoja.

Nahodha wa Panama, Felipe Baloy, amekuwa mmoja wa wachezaji waliofunga bao kwenye michuano ya Kombe la Dunia akiwa na umri mkubwa (miaka37 na miezi minne). Roger Milla kutoka Cameroon aliwahi kufanya hivyo akiwa na miaka 42 na mwezi mmoja.

Kane na Ronaldo ndiyo wachezaji pekee waliofunga mabao matatu katika mchezo mmoja tangu kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi, Ronaldo alifunga dhidi ya Spain na Kane dhidi ya Panama jana.

Baada ya ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Panama jana, England wameendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo hata mmoja kati ya11 iliyopita, wameshinda 8 na sare 3.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic