HABARI NJEMA, BOSSOU AFUNGUKUA KUHUSIANA NA KUREJEA YANGA
Aliyekuwa beki wa zamani wa klabu ya Yanga, Mtogo, Vincent Bossou, amesema kuwa bado hana mkataba na timu yoyote mpaka sasa, imeelezwa.
Bossou ambaye aliwahi kuitumikia Yanga na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17 aliondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kumalizika.
Taarifa zinaeleza kuwa Bossou yupo nchini Vietnam hivi sasa akifanya mazoezi na klabu ya Saigon inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
Imeelezwa beki huyo amesema kama Yanga bado wanahitaji huduma yake, wafanya mazungumzo naye na kama wakifikia makubaliano atarejea Jangwani.
Peleka uhuni wa habari huko. Ulishaandika sana uongo juu yake. Yanga hawamhitaji ana majivuno kama Chirwa.
ReplyDeleteAje afanye nini? Miongoni mwa wachezaji wasumbufu. Aligoma kwenda kucheza na Mediama kisa mshahara .Timu ikafungwa lakini mshahara hakukatwa. Abaki hukohuko
ReplyDeleteWachezaji wa kigeni ni Tshishimbi ,Rostand na Kamusoko ambao wanaipambania timu. Chirwa mahindi yake hayajakauka akavune? Haiwezekani timu ina mechi muhimu wewe hutaki kucheza fukuzia mbali
ReplyDelete