June 22, 2018


Kufuatia Bodigadi wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Mwarabu Fighter aliyepata ajali mbaya alfajiri ya leo katika eneo la Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam na kupasuka kwenye uso, majeruhi huyo ameeleza kuwa kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa huduma ya kwanza katika Hospitali ya Lugalo iliyopo Mwenge jijini Dar kisha kuhamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Akizungumza kwa taabu na Global TV Online akiwa Muhimbili, Mwarabu Fighter anasema alikuwa amepakizwa kwenye bodaboda ambapo dereva wake alikiwa akilipita caterpillar, ghafla mbele yao alitokea dereva mwingine wa bodaboda na kusababisha ajali hiyo.

Anaeleza kwamba alipoteza fahamu kwa zaidi ya dakika ishirini kutokana na kutokwa na damu nyingi lakini anawashukuru madaktari kwa jinsi walivyompigania.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic