June 22, 2018


Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kimesafisha makosa yake iliyoyaonyesha katika mchezo wa kwanza dhidi ya Switzerland kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Costa Rica leo.

Mabao ya Brazil yamewekwa kimiani katika sita za nyongeza kuelekea mchezo kumalizika kupitia kwa Philippe Countinho na Neymar Jr.

Ushindi huo umemfanya Neymar ashindwe kuamini matokeo hayo baada ya kumwaga machozi ya furaha baada ya kufunga bao la pili.

Katika kundi E Brazil imeongoza kwa kuwa na alama 4 ikifuatiwa na Serbia yenye 3 huku Uswizi ikiwa na 1 na Costa Rica wakiwa na 0.

Matokeo hayo yamefuta kiu ya Wabrazil wengi ambao waliponda namna timu yao ilivyocheza mchezo wa kwanza dhidi ya Uswizi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic