HUKU BAADHI WAKIPINGA, TFF YAITAJA KATIBA YA SIMBA INAYOITAMBUA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema inaitambua katiba ya 2014 ya klabu ya soka ya Simba kuwa ndiyo itakyotumika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Simba wanatarajia kufanya uchaguzi ili kupata viongozi wengine watakaoiongoza klabu hiyo kwa miaka minee ijayo kutokana na utawala wa sasa kumaliza muda wake mwezi ujao wa saba.
Kwa mujibu wa Wakili Msomi kutoka kamati ya TFF, Revocatus Kuuli, amesema wao kama TFF wanaitambua katiba ya 2014 na si ya 2016 inayomtaka mgombea Uraisi awe na shahada ama digrii.
Kuuli ameeleza kuwa anajua Simba wapo kwenye mchakato wa kusajili katiba yao mpya kwa msajili mkuu wa serikali lakini inayotambulika hivi sasa ni ile ya zamani ambayo imekuwa ikitumika siku zote pindi uchaguzi wa klabu hiyo unapowadia.
Ikumbukwe baadhi ya wanachama wamekuwa wakipinga suala la katiba kubalishwa huku wakidai kiwango cha elimu ya mgombea kuwa kubwa kutokana na walio wengi kuishia darasa la saba mpaka kidato cha nne.
Mmoja wa wanachama waliosikika hivi karibuni kwenye vyombo vya habari akipinga ni Jamhuri Kihwelo Julio ambaye alilalamika na kueleza kuwa wanachama wengi wa klabu hiyo hawajaenda shule na akiomba kiwango cha elimu kiweze kushushwa kama mwanzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment