June 30, 2018


Mchezaji wa klabu ya JKU, Feisal Salum, maarufu kama Fei Toto, amefunguka na kueleza kuwa anaweza akaelekea Singida United endapo viongozi wa klabu hizo mbili watafikia mwafaka.

Toto ambaye alikuwa anatajwa kujiunga na Yanga amesema kwa sasa viongozi wa JKU wanaendelea kuzungumza na Singida na pale mwafaka utakapofikiwa wakikubaliana ataweza kuondoka.

Kiungo huyo ameonekana kuwa na kipaji cha aina yake ndani ya JKu jambo ambalo limezivuta kwa karibu Yanga na Singida United kunyemelea saini yake.

Yanga nao inaelezwa wapo kwenye mazungumzo na JKU lakini Singida ndiyo wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kumsajili.

Kiungo huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha JKU wakati JKU ikicheza dhidi ya Vipers ya Uganda katika mchezo wa michuano ya KAGAME kwenye Uwanja wa Chamazi Complex na timu yake ikienda sare ya bao 1-1.





2 COMMENTS:

  1. Basi unaona!! Yanga wanasema usajili wao wa sii sasa siri hii ikowapi kila mtu anajuwa na halafu Simba akikupigeni pute mnasema mnaonewa. Hiyo midomo ndio inayokuponzeni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Ndugu hapo alieongea Yanga au Umesoma Kwa Saleh Ally!? Naona Pouvuuuu!!!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic