SINGIDA UNITED YATAMBULISHA SILAHA TATU MPYA KAGAME
Klabu ya Singida United imeshusha silaha zingine tatu zilizoanza kazi katika michuano ya KAGAME CUP jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao wapya ni Hendrik Sombaeb aiyekuwa akiichezea Jomo Cosmos ya Afrika Kusini huku ikielezwa amesaini mkataba wa miaka miwili.
Wakati huo Boniface Maganga aliyekuwa akiichezea Mbao FC msimu uliopita katika Ligi naye ameungana na walima alizeti hao na ikielezwa pia kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili.
Mbali na Maganga, beki aliyekuwa akiichezea Ndanda FC, Ibrahim Job ametambulishwa leo na klabu hiyo kabla ya mchezo wa KAGAME dhidi ya APR ya Rwanda baada ya kumalizana na mabosi wa timu hiyo.
Usajili wa Singida umeonekana kulenga kujenga kikosi kikosi kipya kutokana na kusajili wachezaji wengi mara baada ya nyota wao kutajwa kuondoka ikiwemo Deus Kaseke ukiachana na Tafadzwa Kutinyu ambaye ametimkia Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment