Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, umeziambia timu ambazo zinamhitaji kiungo wao mshambuliaji, Hassan Dilunga kuwa haendi popote.
Dilunga alikuwa na msimu mzuri katika timu ya Mtibwa Sugar na kuisaidia kutwaa ubingwa wa Kombe la FA huku yeye akiibuka kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema kuwa anazishangaa hizo timu zinazomhitaji mchezaji wao kwani bado ana mkataba na timu hiyo, pia hawawezi kumuachia.
“Nilizungumza na Dilunga yeye mwenyewe kuhusu hili, akaniambia kuwa hizi timu zinazomtaka kipindi akiwa Yanga zilikuwa hazimuoni?
"Na lengo lake yeye ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na siyo kurudi tena Simba na Yanga na amesema kuwa ataendelea kusalia kwenye timu yetu kama akiondoka basi ataenda kucheza nje na sisi Mtibwa msimu ujao tunaiwakilisha Tanzania katika michuano ya Shirikisho na ndiyo nafasi yake ya kujionyesha na hatuwezi kumuacha.
“Sisi nguvu kubwa tulielekeza kwenye ligi na kwenye michuano ya FA na baadaye tukaelekeza kwenye Uhai Cup, sasa ndiyo tunataka kukaa kikao na uongozi na kusubiria ripoti ya mwalimu (Zuberi Katwila) kwani bado hajaileta na tumejipanga kufanya usajili mzuri kuleta ushindani wa kimataifa kwani tunaiwakilisha nchi msimu ujao,” alisema Kifaru.
SOURCE: CHAMPIONI
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteYanga wamezizuga timu nyingi wakitumia magazeti kutaja majina ya wachezaji ambazo sio wale ambao kocha huyu mpya anawataka....lakini timu zinafikiri zinaikomoa Yanga kumbe ilikuwa ni zuga. Wawa, dilunga, nchimbi, kaheza, kiyombo (ukiondoa Salamba) hao hawakuwa kwenye listi ya kocha ila walikuwa kwenye listi ya magazeti ya mtaani.....Azam, Singida, Mtibwa, na Simba zote zimeingia chaka 😁

ReplyDeleteTabu yenyewe ni kuwa wachezaji wanafahamu vizuri kuwa wakienda kwa yanga mwisho wa mwezi wataambukia patupu
ReplyDeleteWe kaa ukijidanganya na kujipa moyo kuwa yanga wanazuga wakati hawana pesa za kusajili!
ReplyDelete