June 28, 2018


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema kuwa umempeleka mchezaji wake, Mganda, Juuko Murushid Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio na SuperSport.

Manara amesema kuwa Murushid ameshaelekea Afrika Kusini kufanya majiribio na SuperSport ambayo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo huku matarajio ya Simba ni kuona anafuzu.

Baada ya Murushid kuondoka, Manara amesema Simba imebidi imsajili Pascal Wawa kwa ajili ya kuziba nafasi yake ili hata atakapofanikiwa kusajiliwa na SuperSport nafasi yake iwe tayari imeshazibwa.

Tayari Wawa ambaye ametambulishwa na Simba leo amemalizana na mabosi wa klabu hiyo kwa ikielezwa amesaini mkataba wa miaka miwili.

Hapo awali ilielezwa kuwa Simba wamemtema beki huyo Mganda lakini uongozi umeweka wazi kuwa hajatembwa bali SuperSport walituma ofa kwa ajili ya kumuhitaji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic