WABABE WA SIMBA KUWASILI LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Kikosi cha Gor Mahia kinatarajiwa kuwasili leo nchini kwa ajili ya mashindano ya KAGAME ambayo yameanza jana jijini Dar es Salaam.
Gor Mahia watawasili wakiwa na benchi lao zima la ufundi likiongozwa na Kocha Dylan Kerr aliyewahi kuifundisha klabu ya Simba.
Timu hiyo inatarajiwa kuwasili kuanzia majira ya mchana tayari kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ambayo watakuwa wanakabiliwa nayo katika harakati za kusaka kikombe cha KAGAME.
Gor Mahia wanakumbukwa kwa kuifunga Simba jumla ya mabao 2-0 katika mchezo wa fainali ya mashindano ya SportPesa Super Cup iliyofanyika Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya, wiki kadhaa zilizopita.
Mbali na Gor Mahia, Rayon Sports kutoka Kenya nayo inategemewa kutua leo jijini Dar es Salaam kushiriki michuano hiyo inayoendelea hivi sasa Dar es Salaam.
Wakati Gor Mahia na Rayon zikitarajiwa kufika leo nchini, Simba SC itakuwa inaanza kibarua chake cha kwanza dhidi ya Dakadaha ya Somalia kuanzia saa 8 mchana.
Na baada ya mchezo huo, baadaye AS Ports ya Djbout itakuwa inakabiliana na Lydia Ludic ya Burundi kuanzia saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Chamazi Complex.
0 COMMENTS:
Post a Comment