LOPETEGUi AANZA KUISUKA MADRID, NYOTA MMOJA KUTOKA BAYERN AINGIA KWENYE RADA ZAKE
Akiwa na wiki kadhaa tangu atangazwe kurithi mikoba ya Zinedine Zidane, Kocha mpya wa Real Madrid, Julen Lopotegui amepanga kuchukua nyota mmoja kutoka Bayern Munich.
Kwa mujibu wa Daily Mirror wameeleza kuwa Lopetegu ameanza mchakato wa kufuatilia saini ya Thiago Alcantara ambaye aliwahi kuichezea FC. Barcelona.
Harakati za kumsajili Alcantara zimeanza kufuatia kiungo wake, Mateo Kovacic kuonesha nia ya kutaka kuondoka Real Madrid kwenda mahala pengine.
Usajili huo utakuwa wa pili kwa Lopetegui mara baada ya kumalizana na Mbrazil anayekipiga Santos ya Brazil, Rodrygo Goes ambaye anatarajiwa kujiunga na Madrid hivi karibuni.
0 COMMENTS:
Post a Comment