June 22, 2018


Borussia Dortmund ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Uhispania na Chelsea Alvaro Morata, lakini klabu hiyo ya Bundesliga inaweza ikashindwa kumsajili kutokana na mahitaji ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anayetaka kitita cha £45m(Bild, via Talksport)

Beki wa Uhispania Jordi Alba, 29, anasema kuwa anataka kusalia Barcelona, licha ya hamu kutoka kwa Tottenham. (goal)

Spurs ina matumaini ya kumsajili winger wa Croatia Ante Rebic, 24, huku klabu ya Eintracht Frankfurt ikitaka kumuuza kwa dau la £26.3m. (Bild, via Express)

Juventus inaongoza katika harakati za kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Urusi na CSKA Moscow Aleksandr Golovin, 22, huku Arsenal, Chelsea na Barcelona wakimnyatia. (Tuttosport - in Italian)

Mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri ameanza kupanga kikosi chake cha ukufunzi katika klabu ya Chelsea licha ya hatma ya mkufunzi Antonio Conte kutotatuliwa (mail)

Lucas Torreira anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Sampdoria kwa dau la £26m, huku Arsenal ikimnyatia kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 22-kutoka Uruguay. (Sportitalia, via Mail)

Aston Villa haijapokea maombi yoyote kutoka kwa kiungo wa kati Jack Grealish, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhusishwa na Tottenham na Liverpool. (Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney, 32, ameshauriwa kujiunga na klabu ya ligi ya Marekani DC United na aliyekuwa mchezaji mwenza Steven Gerrard. (Liverpool Echo)

Kiungo wa kati wa Sevilla na Argentina Ever Banega, 29, anataka hakikisho kutoka kwa mkufunzi wa Arsenal Unai Emery kabla ya kukubali kujiunga na klabu hiyo. (La Colina de Nervion, via Mirror)

Beki wa Uturuki na Freiburg Caglar Soyuncu, 22, anataka kujiunga na Arsenal. (Gunes, via Goal)

Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele, 30, anasema kuwa anapenda kujifurahisha na tayari amezungumza na wachezaji wenzake katika kikosi cha Ubelgiji nchini China na ligi ya Marekani MLS. (Goal)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic