June 25, 2018


Michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi inaendelea tena leo kwa viwanja vitatu nyasi zake kuwaka moto.

Nyota Cristiano Ronaldo atakuwa dimbani kuiongoza timu yake ya taifa kukipiga dhidi ya Iran katika mchezo wa Kundi B kwenye Uwanja wa Mordovia kuanzia saa 3 kamili usiku.

Kuelekea mechi hiyo, Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kuonesha ubabe wake wa kucheka na nyavu baada ya kutikisha kamba za wapinzani mara nne katika mechi mbili alizocheza.

Endapo Ronaldo atafunga bao moja dhidi ya Iran atakuwa amemzidi nyota wa England, Harry Kane aliyefikisha mabao matano katika mashindano hayo.

Mechi nyingine zitakazopigwa ni Misri ambao wameshaaga mashindano wakapiga dhidi ya Saudi Arabia majira ya saa 11 jioni huku pia Uruguay wakikipiga na wenyeji Urusi muda huohuo wa saa 11.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic