June 28, 2018


Manchester United wako tayari kumsaini kipa wa klabu ya Stoke ,35, Lee Grant. Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha Uingereza kisichozidi umri wa miaka 21 atatumika kama kipa wa ziada kwa David de Gea na Sergio Romero. (Telegraph)

Mchezaji wa klabu Everton na nahodha wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney, 32, atatia saini mkataba wa miaka miwili na klabu ya DC United katika kipindi cha saa 36 . (Sky Sports)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Napoli Jorginho, 26, anadai kwamba mchezaji huyo anakaribia kukamilisha uhamisho wake hadi Manchester City kwa dau la £43m . (Mirror)


Crystal Palace imempatia kocha Roy Hodgson kandarasi mpya ambayo itamweka katika klabu hiyo hadi 2020. (Sky Sports)

Everton inamnyatia mshambuliaji wa Croatia katika kombe la dunia Ante Rebic. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anaichezea klabu ya Eintracht Frankfurt. (Mirror)

Southampton inakaribia kumsajili mshambuliaji wa basel na Norway Mohamed Elyounoussi, 23. (NBC)

Kutoka BBC


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic