June 28, 2018


Hii sasa sifa. Baada ya kufanikiwa kumalizana na Dida jana ambaye imeelezwa ameshaini mkataba wa miaka miwili, uongozi wa Simba umeanza kuhusishwa kutaka kumsajili kiungo Hassan Dilunga.

Simba imeanza harakati za kuhitaji saini ya mchezaji huyo ambaye ameanza kuhusishwa kwa muda mrefu sasa ili waweze kumrejesha kwenye kikosi chao.

Dilunga ameingia kwenye rada za Simba inayoonekana kusajili vijana na wakongwe kwa ajili ya kukiweka kikosi chake fiti kuelekea mashindano ya kimataifa na Ligi Kuu Bara.

Hapo awali ilielezwa kuwa Yanga walionesha kubaniwa na Mtibwa baada ya kuanza harakati zake za kutaka kumrejesha mchezaji huyo ambaye kabla hajaondoka Yanga alikuwa hapewi nafasi.

Dilunga aling'ara zaidi akiwa na kikosi cha Mtibwa katika Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho kiasi ambacho kinasababisha timu hizo kongwe mbili kuanza mchakato wa kutaka kumsajili.

5 COMMENTS:

  1. Simba mbona ina viungo wengi wataenda kucheza wapi? Mm nashauri kwa ligi ya ndani simba inatosha labda itafute kiungo mwenye nguvu wa kimataifa.. Isiendelee kujaza viungo wa ndani ya nchi ambao kiwango chao kinafanana na hao waliojaa simba.Kina Mo Ibrahim, ndemla,mzamiru,niyonzima wote hawapati nafasi ya kutosha wengine wa nini? Kama walikugharama hawatoshi bora wangewaacha kuliko kuingia gharama kulipa wachezaji ambao hawachezi. #Simba nguvu moja
    #mleteni kahata tuombe mechi ya kirafiki na mazembe englabee.

    ReplyDelete
  2. Simba achaneni na Dilunga. Tafuteni wachezaji ngangari hasa wa kutoka nje.

    ReplyDelete
  3. Dilunga wa sasa kapea ni sawa na mchezaji wa nje Simba wakimchukua powa tu.

    ReplyDelete
  4. simba msajilin baraka lema kutoka nronga fc

    ReplyDelete
  5. Yanga masikini huwa wanajigamba kuwa wanafanya ysajili wao kimya kwa siri halafu hukurupuka kujisifu kuwataja na hapo Simba chapuchapu huwapiga pute kama hapo zamzni walipokuwa wakiwafanyia Simba. Masikini kama wamewekwa kwenye kona wananyofolewa kama vile Simba wanavomnyofoa punda milia. Wajaribu kufunga midomo wasifanye kama vile wana hela ya Mheshimiwa Manji alieingia mitini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic