MKONGOMANI WA YANGA AWAPIGA STOP NYOSSO NA MBENIN, ISHU NZIMA IKO HIVI
Licha ya kamati ya muda ya usajili ya Klabu ya Yanga kuendelea na mipango yake kwa kutumia njia ya kusajili kimyakimya lakini kamati hiyo imeweka wazi kwamba haitamtangaza mchezaji yeyote yule wakimsubiri kocha wao mkuu Mkongo Zahera Mwinyi arudi nchini kuungana na kikosi hicho akitarajiwa kuungana na timu hiyo wikiendi hii.
Kamati hiyo ya muda ya usajili ya Yanga inaundwa na vigogo mbalimbali ikiongozwa na mwenyekiti wake, Abass Tarimba ambapo imekuwa ikifanya kazi yake ya usajili ambao ulipendekezwa na kocha huyo ambaye amechukua mikoba ya Mzambia, George Lwandamina.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Hussein Nyika, amesema kwamba wanaendelea na usajili huo lakini hawataweka hadharani ni nani na nani ambao wamepata saini zao hadi kocha huyo arejee Jumapili hii akitokea nje ya nchi ambapo ameenda kwa shughuli zake mbalimbali kwa kutazama wachezaji hao kama wataendana na matakwa yake.
“Tunaendelea na shughuli ya usajili kwa sasa kwa staili ileile ya kutotangaza ni nani na nani ambao tunawafuatilia au kuwasajili kwa sababu kama tukifanya hivyo tutakuwa tunauza mbinu kwa wapinzani wetu ambao wataenda kuwanasa.
“Hata hivyo, usajili huo ukikamilika bado hatutaweka wazi kwa sababu tutakuwa tunamsubiri kocha Zahera Mwinyi arejee nchini kisha aone jinsi ambavyo tumefanya kisha ndiyo mambo mengine tutayaweka wazi, yeye kwa sasa yuko nje na ataingia nchini Jumapili hii,” alisema Nyika.
Yanga tayari wameshamalizana na straika Marcelin Koupko raia wa Benin lakini bado hawajamtangaza rasmi huku pia wakizifukuzia saini za Juma Nyosso (Kagera Sugar), Mrisho Ngassa (huru) na Mohammed Ibrahim (Simba).
Jana kupitiA Chombo kimoja cha Habari, Mkuu wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika, alisikika akisema Zahera anawasili usiku wa kuamkia leo, hivyo tuone na tusubiri mambo yatakwendaje.
Waandishi wa hii blogu badilikeni kwanini hamwandiki ukweli? Nyosso na Ngassa hawajasajiliwa na Yanga
ReplyDelete