SIMBA WAONA ISIWE TABU, WAAMUA KUMRUHUSU MAVUGO KUELEKEA KLABU HII
Baada ya timu ya Mbao FC kumtaka mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, kuziba pengo la Hababu Kiyombo, uongozi wa timu hiyo umewatoa hofu na kuwataka waende wafanye biashara kwani wao hawana shaka na mchezaji huyo kuondoka.
Mavugo ambaye alijiunga na Simba msimu wa 2016/17 akitokea timu ya Vital’O ya kwao Burundi, amemaliza mkataba na mabingwa hao na sasa ni mchezaji huru kutua timu yoyote.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema kwa sasa hawana papara na usajili wa dirisha kubwa ila kama kuna timu inawahitaji kusajili wachezaji wao waende kuzungumza hawana shida.
“Usajili tuliofanya ni ule wa kina Salamba tu, sisi Mavugo tushamalizana naye mkataba, kama Mbao wanamtaka waje tu wafanye naye mazungumzo kwani ameshamaliza mkataba na sisi,” alisema Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment