June 26, 2018

PATRICK (KATIKATI), AKIWA NA MARCEL KAHEZ (KUSHOTO) NA PAUL BUKABA KATIKA MAZOEZI YA SIMBA KWENYE UWANJA WA BOCCO VETERANI, LEO.


Beki raia wa Nigeria, Victor Patrick ameanza majaribio katika kikosi cha Simba, wakati mmoja sawa beki Pascal Wawa, raia wa Ivory Coast.

Wawa aliwahi kuichezea Azam FC, kabla ya kurejea El Merreikh ya Sudan ambayo kabla alikuwa akiichezea.

WAWA KATIKA MAZOEZI YA SIMBA, LEO.

Kwa sasa Wawa yuko nchini akiendelea kujinoa kuwania kusajiliwa na Simba ambao kidogo walionyesha hofu.

Wakati Wawa ameanza majaribio hayo ya kuwaridhisha Simba kwamba yuko vizuri, Patrick naye alianza jana kuonyesha alichonacho.

Maana yake Simba itakuwa na kazi ya kuchagua kati ya wachezaji hao wawili kutokana na kile watakachokionyesha.

3 COMMENTS:

  1. Viongozi mfanye kweli katika kuchagua yupi ni bora
    #### simba Nguvu moja####

    ReplyDelete
  2. Simba ya Mo kwa sasa haihitaji wachezaji wa majaribio hayo yatakuwa mazingira ya upigaji mwisho tutapata wachezaji miradi ya watu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unahitaji bidhaa ya mchele kwa mfano ni sharti uione; uijue kikamilifu... Otherwise utafungashiwa kisicho..
      Big up uongozi wa Simba.. Anayejiita mchezaji.. Aje aoneshe alichonacho...!!
      Msisajili majina... Sajilini vipaji!!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic