Polisi nchini Argentina wamefanikiwa kunasa rundi la madawa ya kulevya yaliyokuwa yakisafirishwa kutumia makombe ya dunia.
Wasafrishaji waliyaweka madawa hayo ndani ya Kombe la Dunia, yakiwa takribani makombe 10 wakionyesha kuwa yalikuwa yanakwenda kuuzwa nchini Urusi ambako Kombe la Dunia linaendelea.
Hata hivyo kumekuwa na habari tata kwamba kweli yalikuwa yanakwenda Urusi au nchi nyingine lakini ni zaidi ya kilo 30.
Imeelezwa, baada ya polisi katika jiji la Buenos Aires kushitumia mchezo waliyavunja makombe hayo na kukuta Kilo 20 za marijuana au bangi, kilo 10 cocaine safi, dozi1,800 ya cocaine chafuna zaidi ya dola 14,000 zilizokuwa ndani yake.
Kombe hilo maarufu kama Jules Rimet, ndilo linalogombewa kwa sasa nchini Urusi huku Argentika ikisua katika hatua ya makundi. Lakini wauza madawa ya kulevya wamegundua njia mpya ya usafirishaji madawa ya kulevya kwa kuwa wamekuwa wakibanwa kupita kiasi.
0 COMMENTS:
Post a Comment