June 20, 2018


Mwanadada Georgina Rodriguez ameonyesha mapenzi yanaweza kuwa na nguvu na utaifa ukafuatia baadaye.

Georgina ni mpenzi wa nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye leo amefunga bao lake la nne katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi.

Bao hilo la nne amefunga Ureno ikipata ushindi wa kwanza kwa kuitwanga Morocco kwa bao 1-0 huku Georgina ambaye ni raia wa Argentina akisherekea jukwaani akiwa na jezi ya Ureno namba 7 ambayo huvaliwa na Ronaldo.

Kama hiyo haitoshi, Georgina alibeba bender ya Ureno kuendelea kuonyesha anaiunga mkono nchi hiyo aliyozaliwa mpenzi wake.

Hivi karibuni, Ronaldo aliwahi kusema ataiunga mkono pia Argentina wakati wa Kombe la Dunia kwa kuwa mpenzi wake huyo ni mzaliwa na aria wa Argentina.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic