June 20, 2018




Taarifa zinaeleza kuwa ule mpango wa beki wa kati kutoka Ivory Coast, Pascal Serge Wawa ambaye alikuwa kwenye mipango ya kushuka ndani ya kikosi cha Yanga limekwamisha kwa muda mara baada ya klabu hiyo kuunda kamati mpya ya muda ya usajili ambayo inaongozwa na mwenyekiti wake Abass Tarimba.

Wawa alikuwa anpigiwa upatu kwa ajili ya kutua ndani ya kikosi hicho cha Yanga kwa ajili ya kutumika katika michuano ya kimataifa ikiwa ni baada ya kuonekana safu ya ulinzi ya timu hiyo inayumba huku akibaki Kelvin Yondani kuwa nyota pekee kwenye idara hiyo.

Hivi karibuni Yanga katika mkutano wao mkuu waliunda kamati maalum ya kuivusha timu hiyo katika kipindi kigumu, huku pia ikiunda kamati ya usajili ya muda ambayo inaongozwa na Tarimba akiwa na makamu wake Said Mecky Sadik.

Wawa ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya timu ya El Merreikh ya Sudan, amesema kwamba hadi sasa hajaambiwa lolote juu ya yeye kuja ndani ya kikosi hicho licha ya mara ya mwisho kuongea na viongozi wa timu hiyo ambao walimtaka kutuma kivuli (kopi) ya pasipoti yake.

“Kwa sasa ni muda kidogo hawajanitafuta wao kwa ajili ya kukamilisha suala hilo, mara ya mwisho niliongea na baadhi ya viongozi wao na kunitaka niwatumie kopi ya pasipoti kwa ajili ya kunifanyia mipango watume tiketi ya ndege.

“Kwa namna hiyo naona kama dili linaweza kufa kwa sababu zimepita wiki tatu sasa hakuna mawasiliano baina yangu na wao, lakini mimi nipo tayari kwa muda wowote ule wakinihitaji nitakuja kufanya nao kazi,” alisema Wawa.

Mwenyekiti huyo wa kamati ya muda ya usajili Yanga, Tarimba aliwahi kunukuliwa kuwa kamati yao itafanya usajili wa kimyakimya na makini lakini pia wataangalia wachezaji wenye vipaji vya kuichezea timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic