POLAND YAAGA KOMBE LA DUNIA URUSI KWA KICHAPO CHA BAO 3-0 DHIDI YA COLOMBIA
Poland imeyaaga mashindano ya Kombe la Dunia Urusi kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Colombia.
Matokeo ya mchezo huo yamewekwa kimiani na Yerry Mina (40'), Radamel Falcao (70') na Juan Cuadrado dakika ya 75.
Poland inaondoka rasmi kwenye michuano kufuatia kupoteza mchezo wa pili mfululizo baada ya ule kwanza dhidi ya Senegal kuruhusu nyavu zao kufungwa mabao 2-1.
Msimamo wa kundi H unaonesha Colombia wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 3 huku Senegal wakishika nafasi ya pili, wakati Japan wakiwa wa kwanza.
Kuna mengi sana ya kujifunza kwa vijana wetu kwenye mechi ya colombia na Poland. Wakolombia hawakuingia uwanjani kucheza na poland katika hali ya kawaida na kwa upande poland vile vile kwa hivyo ilikuwa vita ya mechi sio mechi ya kawaida. Wakolombia wengi wao wapo fiti hasa kifiziko na ndio kitu amabacho tunasisitiza mara kwa mara kwa vijana wetu wanatakiwa kuwa waendawazimu linapokuja suala la mazoezi hasa yale ya kuujenga mwili kwani mpira wa sasa unahitaji nguvu za kweli sio talenti peke yake. Wakolombia waliweza kuwazibiti wapoland kutokaa na mpira kwa dakika tisini sio kitu rahisi hata kidogo kunahitaji pumzi za kutosha na wachezeji walioiva kimazoezi.
ReplyDelete