June 24, 2018


Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Said Maulid (SMG) amewashauri viongozi wa timu za Tanzania kuhusiana na aina ya wachezaji ambao wanapaswa kuwasajili haswa kipindi hiki dirisha likiwa wazi.

Mchezaji huyo ambaye aliwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa, amesema ifikie wakati wasajili wachezaji ambao wapo kwenye vikosi vya timu zao za taifa.

Maulid anaamini kuwa wachezaji ambao wamechaguliwa katika timu za taifa wanakuwa na uwezo mkubwa wa kuonesha viwango tofauti na wale ambao wapo tu kwenye klabu zao.

SMG ameeleza kuwa kitendo cha timu za Tanzania kufanya hivyo zitasaidia kwa namna moja na nyingine katika soka la kimataifa na ukizingatia hivi sasa klabu kama Yanga ipo kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mbali na Yanga, Simba na Mtibwa nazo zipo kwenye mashindano hayo ambapo zinatarajiwa kuanza vibarua vyao mwezi Disemba mara baada ya ratiba CAF kutoka.

CHANZO: EFM 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic