June 3, 2018


Na George Mganga

Wakati Yanga na JKU zikianza kuiwakilisha Tanzania leo katika ufunguzi wa pazia la michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza mjini Nakuru, Kenya, Simba wao wanafanya mazoezi ya mwisho kuanza kibarua chao kesho dhidi ya Kariobang Sharks.

Simba ambao kikosi chao kimekuwa na mabadiliko kwa kuwa na ongezeko kadhaa la wachezaji, kinajifua mjini Nakuru kujiweka fiti kwa mechi dhidi ya Kariobang Charks itakayopigwa kesho Jumatatu mida ya saa 9 alasiri.

Uongozi wa klabu hiyo umesema hautaipuuzia michuano hii kama walivyofanya mwaka jana na badala yake watapigania kikombe ili wapate nafasi ya kucheza na Everton huko England.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2017/18 wanaenda kuanza mashindano hayo huku wakiwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao.

Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin wote wamesaini miaka miwili kwa ajili ya kuendelea kuitumikia Simba huku kukiwa na ongezeko la wachezaji watatu ambao ni Adam Salamba, Marcel Kaheza na Mohamed Rashid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic