June 25, 2018


Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam leo.

Simba wamezidi kujifua kufuatia ujio wa mashindano ya KAGAME yanayotarajiwa kuanza Juni 29 wiki hii jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi hayo yaliyokuwa chini ya Kocha Msaidizi wa kikosi hicho, Masoud Djuma, yalionekana kunoga zaidi kutokana na uwepo wa beki mpya kutoka Ivory Coast, Pascal Wawa.

Wawa ametua nchini jana na kuhudhuria mazoezi ya Simba ambayo yalifanyika kwenye Uwanja wa White Sand uliopo maeneo ya Mbezi Beach Dar es Salaam.

Beki huyo alionekana mazoezini akiwa bado na ustahimilivu wa hali ya juu sambamba na kuelekewana na kocha Masoud ambaye alikuwa anazungumza naye Kifaransa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic