June 25, 2018


Na George Mganga

Baada ya beki Pascal Wawa kuonekana kwa siku mbili akiwa mazoezini na kikosi cha Simba, uongozi wa klabu hiyo kupitia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Said Tully, ameibuka na kuelezea juu ya uwepo wake.

Tully amesema kuwa ni kweli Wawa amewasili nchini na amejiunga na kikosi hicho ambacho ni bingwa wa ligi kwa msimu wa 2017/18.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia Spoti Leo, Tully huyo amefunguka na kueleza kuhusiana na suala la yeye kusaini mkataba wataliweka wazi mara baada ya michuano ya KAGAME kumalizika.

Wawa amewasili Dar es Salaam jana na kufikia moja kwa moja kwenye Uwanja wa White Sand ambapo Simba walikuwa wanafanyia mazoezi.

Kikosi hicho kimejinoa kwenye Uwanja wa Boko Veterani leo asubuhi huku Wawa akiwa miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi zikiwa zimesalia siku kadhaa kuanza kwa michuano ya KAGAME Juni 29 wiki hii.

7 COMMENTS:

  1. Kama mnasajili kila anayetakiwa na Yanga basi kazi mnayo. Badala ya kusajili kwa mahitaji nyinyi mnakurupuka tu au mnapiga hela za MO?

    ReplyDelete
    Replies
    1. tulia ikuingie

      Delete
    2. WAPI YANGA IMEWEKA ORODHA YA WACHEZAJI INAYOTAKA KUSAJILI HALAFU MKAIKATIA HATI MILIKI? UWE MKWELI TU WACHEZAJI WAPO HURU TIMU YEYOTE KUSAJILI. YANGA INATAKA KUSAJILI DILUNGA WA MTIBWA MBONA HATUJASIKIA SIMBA IKIMCHUKUA? SEMA SIMBA HII SASA NI BALAA MAANA MANULA, WAWA, KAGERE, OKWI, BOCCO, NYONI, KAPOMBE, MKUDE, KOTEI, GYAN,KICHUYA,ASANTE KWASI, SALAMBA, NK NK

      Delete
    3. Bado Tishimbi...ndipo utakapo meza pini bila ya maji...

      Delete
  2. Majina hayachezi mpira kaka bali uwezo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mlisema hivyo kwa Okwi, Boko na Kapombe. Tumezoea maneno yenu ya mkosaji

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic