June 30, 2018


Na George Mganga

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameanza vema safari ya kupigania ubingwa wa michuano ya Kagame baada ya kuitandika bao 4-0 klabu ya Dakadaha kutoka Somalia.

Katika mchezo huo ulipigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba walitawala kwa asilimia kubwa zaidi ya wapinzani wao na kuwapa wakati mgumu kufika langoni, kitu ambacho kilimfanya kipa Ally Salim kutopata kibarua kizito langoni kwake.

Mabao ya Simba yamefungwa na Adam Salamba aliyetikisha kamba za Wasomali mara mbili, huku Marcel Kaheza na Rashid Juma wakifunga bao moja moja.

Kikosi cha Simba kimecheza bila wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kutokana na kupewa mapumziko, wakati huo nyota Meddie Kagere aliyekuwa anasubiriwa kwa hamu na wanasimba wengi akikosekana japo imeelezwa amerejea Kenya kwa muda.

Mchezo mwingine utakaopigwa saa 10 ni AS Ports ya Djibout itakuwa inacheza na Lydia Ludic kutoka Burundi.

5 COMMENTS:

  1. Ha ha ha ha ha ha this is SIMBAAAAAAAA,PIGA KELELEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  2. Hakuna kulala Simba mbele kwa mbele

    ReplyDelete
  3. Hapa lazima niwape heshima Simba na viongozi wake na si kwa ushindi tu bali usajili wao wa mara hii kama utagundua Simba sasa wanatimu ya vijana wenye vipaji vya hali ya juu ndani ya timu yao ya wakubwa ni falsafa safi kabisa na inaonesha jinsi gani simba inavyobadilika ghafla baada ya jitihada za uekezaji. Kuna watu tena wanajiita watu wa mpira wanalalamika na kuponda simba kusajili vijana jamani? Hivyo hatumuoni Kylian Mbape anavyoiteka Dunia kwa kishindo. Cha msingi ni kuwaelimisha na kuwaaminisha vijana wetu kuwa wanaweza kuwa kama Mbape au kuliko ni kujiamini tu na kujituma.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic