June 30, 2018


Timu ya Taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi jioni hii baada ya kuitungua Argentina ikiongozwa na kapteni wao, Lionel Messi kwa bao 4-3, mchezo uliokuwa mkali na wenye hisia miongoni mwa mashabiki.

Ushindi huo waUfaransa umechagiza zaidi na Kylian Mbappe ambaye ametupia kambani mabao mawili huku akisababisha penati ya bao la kwanza.

Ufaransa walikuwa wa kwanza kufunga kunako dakika ya 13 kupitia kwa Antoine Griezmann kwa mkwaju wa penati baada ya Mbappe kufanyiwa madhambi ndani ya boksi kabla ya Angel Di Maria kusawadhisha dakika ya 43. Hadi kipindiu cha kwanza kina malizika, Ufaransa 1-1 Argentina.

Kipindi cha pili, Argentina walianza na kasi ya ajabu ambapo dakika ya 48 walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Gabriel Mercado.

Game ikawa ngumu kwa upande wa Ufaransa, lakini upepo ulibadilika dakika ya ambapo Benjamin Pavard alisawadhisha na kufanya bao kuwa 2-2. Dakika ya 64, Kylian Mbappe akaandika bao la tatu kwa Ufaransa na kabla ya mchezaji huyo kuwamaliza na bao la 4 dakika ya 68.


Argentina walizinduka dakika za mwisho na kufunga bao la tatu kupitia kwa Sergio Aguero dakika ya 90. Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa, Ufaransa 4-3 Argentina.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic