Klabu ya Singida United sasa itakuwa kati ya timu zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Kagame kutokea upande wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga amesema wapokea mwaliko rasmi kuwa moja ya timu zitakazoshiriki michuano hiyo.
“Tunashukuru sana kwa kuwa tumepokea barua rasmi kualikwa kuwa washiriki wa michuano hiyo.
“Tunaamini wameona ushindani tunaoonyesha katika michuano mbalimbali. Kwetu ni jambo zuri na maandalizi yetu pia yako vizuri tu,” alisema.
Tayari Yanga wamejitoa katika michuano hiyo, hivyo Singida inaingia kama wawakilishi wa Tanzania wanaotarajiwa kufanya vema.
0 COMMENTS:
Post a Comment