June 21, 2018


Nyota anayeongoza katika upachikaji wa mabao kwenye michuano ya Kombe la Dunia hivi sasa nchini Urusi, Cristiano Ronaldo, ameripotiwa kuhitaji kitita cha pauni milioni 1.35 ili kurejea Manchester United.

Ronaldo amabaye anakipiga katika klabu ya Real Madrid Spain, ameanza vema mashindano ya Kombe la Dunia kwa kufunga mabao manne pekee ndani ya mechi mbili ikiwa ni matatu dhidi ya Spain na moja dhidi ya Morocco.

Kutokana na kiwango cha mchezaji kutoonekana kuchuja, inaelezwa kuwa sasa amewataka mabosi wa Manchester United kujiweka sawa ili kumpa mpunga huo kama mshahara wake kwa wiki endapo atajiunga na mashetani hao wekundu.

Mshahara anaolpigwa Ronaldo kwa sasa na Madrid ni pauni milioni 350,000 huku mpinzani wake anayekipiga FC. Barcelona, Leo Messi akilipwa 673,000 kwa wiki pia.

Ronaldo amehitaji kiasi hicho cha pesa ili kuwazidi baadhi ya mastaa waliomuacha kwa kupokea kiwango kikubwa cha mshahara ikiwemo Neymar Jr anayeichezea PSG ambaye analipwa pauni 619,000 kwa wiki.

Aidha ripoti pia zimeeleza kuwa Ronaldo amekuwa hana furaha juu ya mshahara anaolipwa na Madrid kwa sasa, na ikielezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa baada ya michuano ya Kombe la Dunia akarejea kujiunga na timu yake ya zamani Man united.

Kufuatia kuipachikia timu yake ya Ureno mabao manne ikiwa ni baada ya kufunga moja dhidi ya Morocco jana, timu hiyo tayari imeshatinga hatua ya 16 bora hivi sasa ikiungana na wenyeji Russia iliyowaondoa Mafarao wa Misri kwa mabao 3-1.

1 COMMENTS:

  1. hbr kama hiz zifanyien utafiti. ureno bado haijafuzu kuingia mtoano had mechi ya mwisho ndo itakayoamua..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic