June 21, 2018


Uongozi wa klabu ya Singida United kupitia kwa Mkurugenzi wake, Festo Sanga, umethibitisha kupokea barua ya CECAFA yenye ombi la kuwahitaji washiriki mashindano ya KAGAME.

Sanga amesema kuwa ni kweli wameshaipokea barua hiyo na wakitoa shukrani zao kwa viongozi wa CECAFA kutokana na awali waliwahi kuwaomba wajumuishwe pia kwenye mashindano hayo.

Nyika amefunguka na kusema ni furaha kwao kwakuwa wana malengo mazuri na mashindano hayo ya kukitengeneza vizuri kikosi chao kutokana na kuwa na rundo la wageni wengi.

Mbali na kukitengeneza, Nyika ameeleza wanaenda kupigania ushindi na ikiwezekana kutwaa kikombe ili kujijengea heshima kwenye mashindano hayo pamoja na mkoa wa Singida kwa ujumla.

Michuano hiyo inayoanza Juni 28, Singida wao wataanza kibarua chao dhidi ya APR ya Rwanda Juni 29 2018 ikiwa ni mechi yao ya kwanza katika mashindano hayo.


2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic