MKONGOMANI WA YANGA KUREJEA USIKU HUU KUANZA MAANDALIZI YA DOZI KALI DHIDI YA GOR MAHIA
Na George Mganga
Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera, anatarajiwa kuwasili nchini usiku huu akitokea kwao Congo baada ya kwenda mapumzikoni.
Zahera anarejea Tanzania kwa ajili ya kuanza maandalizi mapema ya kukabiliana na Gor Mahia FC kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Mkuu wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Yanga, Hussein Nyika, amethibitisha urejeo wa Zahera ili kuanza kunoa vijana wake wanaotarajiwa kuanza kuwasili wiki ijayo.
Nyika ameeleza kuwa wachezaji wote wa Yanga wataanza kuwasili wiki ijayo kwa ajili ya kuanza kazi maalum ya kuwawinda Gor Mahia FC.
Mchezo wa mkondo wa kwanza utaanza kupigwa jijini Nairobi ambapo Yanga watakuwa wageni dhidi ya mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini humo.
0 COMMENTS:
Post a Comment