Utakuwa unamkubuka huyu kinda Rashid Juma. Alianza kung’ara na Simba katika mechi za mwisho kabisa za Ligi Kuu Bara.
Alisababisha penalti katika mechi ya mwisho dhidi ya Majimaji. Lakini akaonyesha cheche zake katika SportPesa Super Cup.
Kijana yuko vizuri asee. Sasa anataka kuanza msimu kwa kasi na ameanza kuonyesha anataka namba baada ya kumgalagaza beki Serge Paschal Wawa.
Beki mpya wa Simba, anajulikana kwa ukatili lakini JUma amemchukua, akamzungusha na kumuacha akizubaa chini.
Hii ilikuwa ni katika mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Boko Veterani, jana.
Ilikuwa vigumu kuamini kama aliyelamba nyasi ni Wawa na aliyefanya hivyo ni kinda Juma ambaye anaonekana akilelewa vizuri, basi Simba watakuwa wamezalisha “silaha ya maangamizi.”
kwa hiyo unamaanisha ni bomu hebu jaribu kuandika vitu vyenye tija wewe mwandishi acha uyanga
ReplyDelete