June 11, 2018


Kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Nabil Fekir, 24, alikuwa na matumaini makubwa kuwa kuhama kwake kwenda Liverpool kungekamilika kiasi kwamba alikuwa tayari amechagua namba ya shati lake. (L'Equipe, via Star)

Kipa wa Roma Alisson, 25, yuko na furaha sana huko Roma licha ya Liverpool kummezea mate kwa mujibu wa kocha wake Claudio Tafferel. (Tele Radio Stereo, via Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 28, atasalia klabu hiyo hadi meneja mpya ateuliwe licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kumsaini. (Independent)

Paris St-Germain wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Chelsea mfaransa N'Golo Kante 27, ambaye ajenti wake amekutana na mkurugenzi wa ligi nambari moja. (Paris United, via Sun)

Arsenal wanakaribia kumaliza kumsaini beki wa Freiburg na Uturuki Caglar Soyuncu , 22, baada ya ajenti wake kuthibitisha kuwa mazungumzo yamefanyika. (Turkish Football, via Sun)

Baada ya Fabinho, Liverpool wakaribia kumnunua mchezaji mwingine nyota
Beki wa Barcelona Joel Lopez, 15, amefikia makubaliano na Arsenal. (Sport)

Beki wa Italia Leonardo Bonucci, 31, anasema hana tatizo lolote huko AC Milan baada ya kuhusishwa kwenda Manchester United. (Sky Sport Italia, via Mail)

Real Madrid wanaandaa ofa ya pauni milioni 132 kumnunua kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic.

Mchezaji huyo wa miaka 23 pia anamezewa mate na Manchester United. (Il Messagero, kupitia Express)

Huenda Newcastle wasimwinde mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish ambaye thamani yake inawekwa kuwa pauni milioni 30. (Chronicle)

Kutoka BBC

1 COMMENTS:

  1. Baada ya Fabinho, Liverpool wakaribia kumnunua mchezaji mwingine nyota
    Beki wa Barcelona Joel Lopez, 15, amefikia makubaliano na Arsenal. (Sport) Hii taarifa inamaanisha nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic