UKIACHANA NA MARTIN KUELEZWA ANAHITAJIKA UBELGIJI, UONGOZI YANGA WASEMA WAPO WENGINE WANNE
Na George Mganga
Ukiachana na taarifa zilizoeleza kuhusiana na mchezaji, Emmanuel Martin kuhusishwa kuwania na klabu ya Waasland Beveren inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji, uongozi Yanga umefunguka na kusema wapo wengine wanaohitajiwa.
Kupitia Mweyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika, amesema kuwa si Martin pekee anayehitajika na klabu za nje bali kuna wengine wanne.
Kupitia mahojiano yaliyofanywa na Radio EFM, Nyika ameshindwa kuweka wazi suala la Martin kuhitajika na Beveren huku akiowomba wapenzi na wanachama wa Yanga kuzidi kuvuta subira juu ya taarifa hizo mpaka pale wakati mwafaka utakapowadia.
Mbali na Martin, Nyika ameeleza wachezaji wengine wanne wanawindwa lakini akishindwa kuwataja pamoja na timu ambazo zinawanyemelea hivi sasa.
Taarifa hizi za wachezaji hao kuhusishwa kuondoka zimezidi kushika kasi wakati timu hiyo ikikabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC Julai 18 2017.
Tayari Yanga imeshaachana na Donald Ngoma ambaye waliamua kuvunja naye mkataba na kutimkia Azam FC na baadhi bado wanahusishwa kuelekea pengine.
0 COMMENTS:
Post a Comment