June 21, 2018


Bao pekee la Kylian Mbappe limewafanya Ufaransa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Peru katika mchezo wa kundi C kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.

Mbappe amefunga bao hilo akiwa na umri mdogo zaidi kwenye michuano hiyo mnamo dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza na kudumu dakika zote za mchezo.

Mchezaji huyo anayeichezea PSG ya Ufaransa amefunga bao hilo la kwanza ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano hayo akiwa na umri wa miaka 19 na miezi 6 pekee.

Matokeo yanaifanya Ufaransa kuwa ya kwanza katika kundi C ikiwa na alama 6 baada ya kushinda mechi zote mbili na kuwaacha kwa alama mbili Denmark walio nafasi ya pili na alama 4.

Baadaye Argentina ya Lionel Messi itakuwa kibaruania kukipiga na Croatia kwenye mchezo wa kundi D

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic